Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2016



Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha   Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa  niaba ya Rais  Dk John Pombe Magufuli.

Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi  pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.

Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,mifugo na uvuvi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamad Rashid.
Posted by MROKI On Sunday, August 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo