Nafasi Ya Matangazo

November 19, 2015

Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania. 
******


Na Father Kidevu
Rais Dk John Pombe Magufuli amempendekeza Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa  kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tano.



Jina la Kassim Majaliwa lilifikishwa kwa Spika na Mpambe wa Rais (ADC) na kupokelewa na Spika wa Bunge Job Ndugai ndani ya Bunge na baada ya mjumbe huyo maalum wa Rais kutoka ndipo Spika wa Bunge akisaidiana Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila walifungua bahasha hiyo kutoa jina lakini lilikuwa ndani ya bahasha nyingine mbili zaidi hadi alipokuta kadi maalum ambayo iliandikwa kwa mkono jina la mteule huyo wa Rais.



Baada ya kusoma kile ambacho Rais alikiandika ndipo Bunge likaenda mapumzikoni na likarejea kwaajili ya kuthibisha jina hilo kuwa Waziri Mkuu kwa kupiga kura ambapo kati ya wabunge 351 walioshiriki kazi hiyo wabunge 258 sawa na asilimia 73.5 waliridhia huku 91 wakisema HAPANA na kura mbili kuharibika.



Akizungumza muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kumtangaza rasmi kuwa Waziri Mkuu mpya, Kassim Majaliwa alitoa neno la shukrani ambapo aliwashukuru wabunge wote kwa ushindi huo waliompa lakini akisisitiza kuendeleza ushirikiano baina yao katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.



Majaliwa pia ameahidi kufanya zira katika majimbo ya wabunge wote na kuangalia changamoto zinazowakabili majimboni humo na maendeleo yaliyofikiwa pamoja na kuwasikiliza wananchi wanasema nini.



“Mheshimiwa spika niwashukuru wabunge wenzangu wote wote kwa kuridhia kwa kulipigia kura nyingi jina langu ambalo limeletwa kwenu na Mheshimiwa Rais ilimuweze kuridhia tuweze kufanya kazi ya pamoja kwa watanzania nawashukuru sana sana sana nataka niwahakikishie pamoja na shukurani hizi kwamba nitawapa ushirikiano wa hali ya juu wote bila kujali vyama vyenu nyie wote ni wawakilishi wa wananchi wa watanzania tutafanya kazi kwa pamoja ya ufuatiliaji wa shughuli zote za maendeleo za kuisimamia pia na serikali yetu na mimi niseme nitasikiliza pia ushauri wenu katika kufanya kazi za kila siku,” alisema Majaliwa. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Aliongeza kuwa “Nawafahamu vizuri wale ambao mnaendelea na Bunge hili tumefanya kazi pamoja kwa miaka mitano iliyopita tunaendelea kushirikiana tunaendelea kushauriana tunaendelea kufanya kazi kwa watanzania wenzetu na bado niwahakikishie kwamba tutaendelea na wajibu uleule wa kufanya kazi kwaajili ya kuleta maendeleo ya taifa letu, nawashukuru sana waheshimiwa wabunge kwa kuridhia jina langu.”



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anataraji kuapishwa kesho katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma,katika sherehe zitakazo hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wabunge.



Majaliwa alizaliwa Desemba 22,1960 huko Wilayani Ruangwa mkoani Lindui na kluapata elimu ya msingi Mnacho kuanzia mwaka 1970 hadi 1976 ambapo mwaka 1977 alijiunga na sekondari ya Kingonsera ambapo alihitimu kidato cha nne 1980. Mwaka 1991 alijiunga na chuo cha ualimu Mtwara hadi mwaka 1993 mwaka uliofuata 1994 alijiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi 1998.



Mwaka 1999 alikwenda nchini Sweden kwa masomo katika chuo cha Stockhom.



Majaliwa amepata kuwa mwalimu katika shule mbalimbali, amekuwa Katibu wa Cghama cha walimu mkoa wa Singida, kabla ya mwaka 2006 kuteuliwa na Rais Jakaya Kiwete wa awamu ya nne kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo na baade kuhamishiwa Wiklaya ya Rufiji.



Aliamua kuingia katika siasa mwaka 2010 na kugombea ubunge jimbe la Ruangwa na kushinda kiti hicho na baade kuteuliwa kuwa Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (ELIMU) wadhifa aliodumu nao kwa miaka 5.
Posted by MROKI On Thursday, November 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo