Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
******
******
Na Father Kidevu
Rais Dk John Pombe Magufuli
amempendekeza Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya
tano.
Jina la Kassim Majaliwa
lilifikishwa kwa Spika na Mpambe wa Rais (ADC) na kupokelewa na Spika wa Bunge
Job Ndugai ndani ya Bunge na baada ya mjumbe huyo maalum wa Rais kutoka ndipo
Spika wa Bunge akisaidiana Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila walifungua
bahasha hiyo kutoa jina lakini lilikuwa ndani ya bahasha nyingine mbili zaidi
hadi alipokuta kadi maalum ambayo iliandikwa kwa mkono jina la mteule huyo wa
Rais.
Baada ya kusoma kile ambacho
Rais alikiandika ndipo Bunge likaenda mapumzikoni na likarejea kwaajili ya
kuthibisha jina hilo kuwa Waziri Mkuu kwa kupiga kura ambapo kati ya wabunge
351 walioshiriki kazi hiyo wabunge 258 sawa na asilimia 73.5 waliridhia huku 91
wakisema HAPANA na kura mbili kuharibika.
Akizungumza muda mfupi baada
ya Spika wa Bunge kumtangaza rasmi kuwa Waziri Mkuu mpya, Kassim Majaliwa
alitoa neno la shukrani ambapo aliwashukuru wabunge wote kwa ushindi huo
waliompa lakini akisisitiza kuendeleza ushirikiano baina yao katika kuwaletea
wananchi wa Tanzania maendeleo.
Majaliwa pia ameahidi kufanya
zira katika majimbo ya wabunge wote na kuangalia changamoto zinazowakabili
majimboni humo na maendeleo yaliyofikiwa pamoja na kuwasikiliza wananchi
wanasema nini.
“Mheshimiwa spika niwashukuru
wabunge wenzangu wote wote kwa kuridhia kwa kulipigia kura nyingi jina langu
ambalo limeletwa kwenu na Mheshimiwa Rais ilimuweze kuridhia tuweze kufanya
kazi ya pamoja kwa watanzania nawashukuru sana sana sana nataka niwahakikishie
pamoja na shukurani hizi kwamba nitawapa ushirikiano wa hali ya juu wote bila
kujali vyama vyenu nyie wote ni wawakilishi wa wananchi wa watanzania tutafanya
kazi kwa pamoja ya ufuatiliaji wa shughuli zote za maendeleo za kuisimamia pia
na serikali yetu na mimi niseme nitasikiliza pia ushauri wenu katika kufanya
kazi za kila siku,” alisema Majaliwa. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Aliongeza kuwa “Nawafahamu
vizuri wale ambao mnaendelea na Bunge hili tumefanya kazi pamoja kwa miaka
mitano iliyopita tunaendelea kushirikiana tunaendelea kushauriana tunaendelea
kufanya kazi kwa watanzania wenzetu na bado niwahakikishie kwamba tutaendelea
na wajibu uleule wa kufanya kazi kwaajili ya kuleta maendeleo ya taifa letu,
nawashukuru sana waheshimiwa wabunge kwa kuridhia jina langu.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
anataraji kuapishwa kesho katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani
Dodoma,katika sherehe zitakazo hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na
serikali pamoja na wabunge.
Majaliwa alizaliwa Desemba
22,1960 huko Wilayani Ruangwa mkoani Lindui na kluapata elimu ya msingi Mnacho
kuanzia mwaka 1970 hadi 1976 ambapo mwaka 1977 alijiunga na sekondari ya
Kingonsera ambapo alihitimu kidato cha nne 1980. Mwaka 1991 alijiunga na chuo
cha ualimu Mtwara hadi mwaka 1993 mwaka uliofuata 1994 alijiunga na chuo Kikuu
cha Dar es Salaam hadi 1998.
Mwaka 1999 alikwenda nchini
Sweden kwa masomo katika chuo cha Stockhom.
Majaliwa amepata kuwa mwalimu
katika shule mbalimbali, amekuwa Katibu wa Cghama cha walimu mkoa wa Singida,
kabla ya mwaka 2006 kuteuliwa na Rais Jakaya Kiwete wa awamu ya nne kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Urambo na baade kuhamishiwa Wiklaya ya Rufiji.
Aliamua kuingia katika siasa
mwaka 2010 na kugombea ubunge jimbe la Ruangwa na kushinda kiti hicho na baade
kuteuliwa kuwa Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (ELIMU) wadhifa
aliodumu nao kwa miaka 5.
0 comments:
Post a Comment