Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2015

Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza nao, kuhusu mafanikio na matarajio ya shirika, wakati akijitambulisha, Dar es Salaam jana. 
**************
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Ndege la Kimataifa Emirates lenye makao yake makuu Dubai, jana lilimtangaza Meneja wake mpya wa Tanzania Bw. Husain Alsafi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafLa fupi ya utambulisho wake Mtendaji huyo mpya wa Emirates Bw. Husain Alsafi alisema kwamba, Emirates imefanikiwa kufikia wastani wa asilimia 12% wa idadi ya wateja wake wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mtendaji huyo mkuu aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Shirika hilo la Ndege la kimataifa linatimiza matakwa ya abiria wake hasa kwa soko la Tanzania na kwingineko, hivyo basi wameahakikisha kuwa na safari za kila siku kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kupitia Dubai, hivyo watanzania wengi wananufaika pale wanapotumia kusafiri na shirika hilo ambapo pia wanapata faida Zaidi endapo watapanga safari zao mapema ili kupata punguzo la bei/nafuu Zaidi.

Katika kushiriki kwake Tanzania Mtendaji huyo MKuu alisema kuwa wametoa kipaumbele kikubwa kwa wazawa ambapo katika kuajiri wamefanikiwa kuwa na watanzania Zaidi ya 30 katika shirika hilo na pia wanazidi kuongeza  idadi ya Watanzania ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi Zaidi.

“ Emirates Tanzania imefanikiwa kuajiri watumishi wengi sana kutoka hapa hapa nyumbani ikiwa ni mojawapo ya vipaumbele vyetu katika kila nchi husika na pia tunaendelea kutoa nafasi  mbali mbali Zaidi”, alisema Bw. Alsafi.

Kuhusu kupanua vituo Mtendaji huyo alisema kuwa Emirates imeendelea kuwa kivutio cha utalii duniani kwote kwa njia mali mbali ikiwa ni pamoja na kuongeza/kupanua vituo vyake sehemu mbali mbali ambapo kwa mwaka huu hali hiyo imepelekea kukua kwa soko lao hasa kwa nchi kama vile India, UK, Amsterdam, China na France, sehemu ambazo watalii wengi wamekua wakivutiwa Zaidi pindi wanapofanya safari zao kupitia shirika hilo la Ndege.

Akizungumzia kwa upande wa kusafirisha mizigo mbali mbali aliongeza kuwa Emirates imekua ikifanya kazi kwa ukaribu sana hasa na wakulima wa Tanzania kwa muda mrefu sana, ambapo kupitia kitengo cha Sky Cargo kimekua mstari wa mbele katika kutimiza hilo na kuhakikisha usalama wa mizigo ya watu pia kuwafikishia kwa muda uliopangwa, kuwaunganisha wafanya biashara kutoka Tanzania na wale walioko nchi zingine kama Arabuni (UAE) n.k. kudhamini Watanzania wanaozalisha na kusafrisha bidhaa zao za chakula katika maonyesho Dubai. 

Wanawapatia nafasi ya kukutana na kuzungumzia maendeleo a wanunuzi mbalimbali ulimwenguni.
Posted by MROKI On Tuesday, September 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo