Ajali imetokea mapema leo Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya ambapo Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukuia kwenye Mto Kiwira
mapema na watu 19 wamepoteza Maisha.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi
yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster)
kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo
baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace
hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.
Inaelezwa
kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva
wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.
Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.
Maiti zikiwa zimetolewa eneo la ajali mtoni.
Hapa ndipo gari hilo lilipo acha njia na kutumbukia mtoni.
0 comments:
Post a Comment