Nafasi Ya Matangazo

March 14, 2015


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo (mwenye kofia), ambayo kampuni yake inakarabati barabara ya Mwai Kibaki eneo la Msasani Dar es Salaam jana. Wengine ni Wataalamu wa barabara Manispaa ya Kinondoni. 
 Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo (mwenye kofia wa pili kulia), akitoa maelezo kwa DC Makonda.
 DC Makonda (wa kwanza kushoto), akizungumza na wakazi wa Msasani kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira.
 DC Makonda akikagua mitaro inayojengwa na Kampuni ya Delmonte (T) Ltd.
 DC Makonda akiangalia mfereji unaotiririsha maji taka kutoka Hospitali ya TMJ.
 Fundi bomba wa Hospitali ya TMJ, Mansoul Mramba akitoa maelezo kwa DC Makonda kuhusu utiririshaji wa maji taka hayo.
DC Makonda (wa pili kulia akinagalia maji taka eneo la Msasani karibu na Ofisi za Tanesco Wilaya ya Kinondoni.

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ametoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuacha kutiririsha maji taka kwenyenda barabarani na kwenye makazi ya watu.

Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushitukiza ya kukagua barabara, madaraja na miundombinu eneo la Msasani ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hasa wakati wa mvua za masika.

"Natoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ kuhakikisha wanaacha kutiririsha maji taka kutoka katika hospitali hiyo kinyumbe cha agizo langu zitafuata hatua kali za kisheria" alisema Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda aliwataka wakazi wa eneo hilo la Msasani kuacha kutupa takataka kwenye mitaro ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kuziba kwa mitaro hiyo na kuwa mtu yeyote atakayebainika akitupa taka taka hizo atachukuliwa hatua kali.

Makonda alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga na kutengeneza barabara lakini watu wachache wamekuwa wakiharibu kwa kutupa taka taka hovyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Posted by MROKI On Saturday, March 14, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo