Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu saba kwa kosa la kujihusisha na upigaji
Ramli chonganishi na imani za ushirikina. Katika msako maalum uliofanyika
kuanzia tarehe 09/03/2015 Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.
Akithibitisha
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
DAVID A. MISIME – SACP aliwataja watu waliokamatwa pamoja na Nyara za Serikali
wanazotumia kupiga Ramli chonganishi kuwa ni DAUD MNYETUMBI, Mwenye umri wa
miaka 70, mkulima wa Chanhumba – Ilolo, Kata ya Handali, alikamatwa akiwa na Ngozi
moja ya fisi, Ngozi moja ya kenge,
Kipande cha Mkia wa Twiga, Pembe ya Digidigi na Kioo.
Mtu
wa pili ni ERNEST TOGOYA, mwenye umri wa miaka sabini (70), Mkulima wa
Chanhumba kitongiji cha Sasajila, Kata ya Handali. Alikamatwa akiwa na; Ngozi moja
ya nyoka aina ya Swila, Jino moja la Ngiri, Pembe ya ng’ombe, vipande viwili
vya ngozi ya ngo’ombe (viatu vya ramli na ndoto za kichawi).
Mtu
wa tatu ni ANTONY KASUGA, Mwenye umri wa miaka arobaini na saba (47), Mkulima
wa Chanhumba - Ilolo, Kata ya Handali. Amekamatwa akiwana na; Ngozi moja ya
Mbweha, Ngozi tatu za nyoka, mbili za aina ya swira na moja ya Chatu, Mkia wa
Fisi, Jino moja la Ngili, Gamba la Kakakuona, Ngozi ya Fungo na vipande viwili
vya ngozi ya ng’ombe (viatu vya ramli na ndoto za kichawi).
Mtu
wa nne ni ROBARTI TALIBO, Mwenye umri wa miaka hamsini na nne (54), Mkulima wa
Kata ya Handali kijiji cha Malechela. Amekamatwa akiwa na Ngozi moja ya Mbweha,
Mkia wa Ng’ombe na Vioo viwili.
Mtu
wa tano ni MALIMA MATUNGWE, Mwenye umri wa miaka sitini na mbili (62), Mkulima
wa Kata ya Mvumi kijijij cha Malechela.
Amekamatwa akiwa na Ngozi ya Nyoka aina ya Swira mbili, Ngozi ya Kenge na Mkia
wa Nyumbu.
Mtu
wa sita ni MTEMI SUMILE, Mwenye umri wa miaka sabini na tano (75), Mkulima wa
Kata ya Mvumi Mission kijiji cha Chihembe. Amekamatwa aikiwa na; Vipande vya
ngozi ya ng’ombe (viatu vya ramli na ndoto za kichawi) pamoja na Kioo kimoja.
Mtu
wa saba ni LUSINDE MCHETE, Mwenye umri wa miaka tisini (90), Mkulima wa Kata ya
Mvumi Mission Kitongoji cha Jamhuri. Amekamatwa akiwa na; Mwiko wa kupigia
ramli, Pembe la Ng’ombe na vipande viwili vya ngozi ya ngombe vya ramli na
ndoto za kichawi.
Uchunguzi
zaidi unaendelea na Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara utakapokamilika kwa
makosa ya Kupatikana na nyara za Serikali na Kijihusisha na upigaji ramli
chonganishi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME – SACP ametoa wito kwa wananchi
kuondokana na tabia ya baadhi ya watu kujihusisha na imani za kishirikina na
kupiga ramli kwani ndizo baade hupelekea watu wenye ualbino kuuawa na kukatwa
viungo; Pia vikongwa kuuawa kwa imani kwaba wanazuia mvua isinyeshe au wanaloga
watu.
Kila
mmoja atambue kuwa unachomfanyia mwingine kwa imani potofu za kiushirikina na
kiuchonganishi kinaweza kesho au kwa siku za baadae kikakupata wewe au mtu wa
familia yako; Tunatakiwa wote kuanzia ngazi ya familia kupeana elimu na kupiga
vita mabo hayo.
0 comments:
Post a Comment