Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2014

Polisi akiingia bora
Baadhi ya Polisi wa doria ya Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora.
*****
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamepora begi linalodaiwa kuwa na fedha kisha kumpiga risasi ya shingo mwendesha boda boda na kupora pikipiki yake nje ya Kiwabnda cha Bora, baranara ya Njerere Dar es Salaam mchana huu.

Father Kidevu Blog ilifika eneo la tukio na kukuta watu wakielezea tukio hilo na kulifabnanisha na la sinema kutokana na kile walichokiona.

"Tuliona mzee mmoja tunahisi ni mfakazi wa Bora, alifika na pikipiki hapa, wakati anataka kuingia ndani wakafika watu wengine wawili katika pikipiki na kuamuru kupewa begi lile na ghafla mwenda pikipiki akawa anawahoji inakuaje wanachukua begi hilo ndipo tukasikia mlio wa risasi na bodaboda yule akaanguka chini wakamsukuma na kuchukua pikipiki yake na kukimbia nayo," alisema shuhuda yule.

Polisi ilifika eneo la tukio huku wengine wakiendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu hao wakutumia sihala huku hofu ya kijana yule wa boda boda kupoteza maisha ikiwa kubwa kutokana na eneo alilopigwa risasi.
Posted by MROKI On Friday, October 17, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo