KIKOSI
cha Yanga kesho kinatarajia kuendelea na maandalizi ya Ligi Kuu kwenye uwanja
wa Shule ya Sekondari Loyola, na Alhamisi itasafiri kuelekea Morogoro kwa ajili
ya mchezo wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kwenye
uwanja wa Jamuhuri Jumamosi.
Washindi
hao wa mchezo wa Ngao ya Jamii leo wamepumzika baada ya jana kutoa kipigo cha
mabao 3-0 dhidi ya bingwa wa msimu uliopita Azam kwenye mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mabao yaliofungwa na Geilson Santos ‘Jaja’
na Simon Msuva.
Meneja
wa Yanga Hafidh Salehe,amesema katika kikosi kitakacho elekea Morogoro Alhamisi
atakuwemo kiungo Mbrazili aliyekosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam
Andrey Coutinho,baada ya kupona maumivu hayo.
0 comments:
Post a Comment