Nafasi Ya Matangazo

July 15, 2014

 Duka la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Kazi za uokoaji zikiwa zimeanza huku wasamalia wema wakisaidia kuhamisha vitu
 Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
 Baadhi ya vyombo na vifaa vya duka la kushonea nguo vikiwa vimeokolewa
 Kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea
 Moshi Mkubwa uliowachanganya watu na kila mmoja kuanza kutaka kukimbia eneo la tukio
Vijana wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
 Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
 Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
 Upande mwengine wa mashuhuda
 
 Vijana wakiwa bize wanafanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
 Vijana wakiwa wanashughulika kwa nguvu zote ili wapate kuzima moto mara moja
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
 Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji
 Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
 Kazi ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto huo.

*******
Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.

Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.

Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia kuteketea vibaya kwa moto huo.
Posted by MROKI On Tuesday, July 15, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo