Mtoto
wa muigizaji mkongwe nchini, Mzee Small, Wangamba Mahmud Said Wangamba
ameiomba serikali na makampuni aliyoyafanyia kazi baba yake kumsaidia
gharama za matibabu ya baba yake yaliyosimama kwa sasa kutokana familia
hiyo kushindwa kumudu.
Akizungumza
na mtandao wa filamucentral, Mahmud alisema familia imeshindwa
kuendeleza matibabu ya Mzee Small kwa muda mrefu kutokana familia hiyo
kuwa na kipato kidogo na kushindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo
kuiomba serikali na makampuni aliyowahi kufanyanayo kazi yaweze
kumsaidia.
“Sisi
kama familia tunajisikia vibaya sana tunaposhindwa kumsaidia baba kwa
sababu yeye ni kila kitu, mimi nasoma sina kipato, mzee toka mwaka jana
mwezi wa tano mwaka jana alipomaliza dawa zake hajatumia dawa hadi leo
kwa sababu hatuna fedha,”
“Lakini
jambo linalotuuma hakuna hata kampuni ambayo imeonyesha kumsaidia kama
Bakhresa alikuwa kuwa akifanya nao kazi hakuna msaada lakini pia
Serikali kupitia menejimenti utumishi wa umma walikuwa wanafanya nao
kazi wamemtosa yupo tu, pengine wanasubiri afe ndio waje
kumzika,”anasema Mahmud.
Mzee
Small anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ikiwa sambamba na kupoteza
kumbukumbu anahitajka zaidi ya milioni moja na nusu kwa ajili ya
matibabu kutokana na ushauri wa daktari kwani inasemekana kichwani kuna
tatizo ambalo linamsababishia kupoteza kumbukumbu anahitaji dawa kwa
ajili ya tatizo hilo na muda wa kupomzika.
Kwa
anayeguswa na tatizo hilo anaweza kuitumia familia yake mchango wa
matibabu kwa namba TIGO – PESA 0714 344 039 kumsaidia mzee Small.
Source: Filamu Central
0 comments:
Post a Comment