Mshauri
mkuu wa vipindi vya Radio 5 David Rwenyagira akiongea na vyombo vya
habari jana kuhusu Tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kuanza
rasmi tarehe 14/10/2013 jijini hapa lenye lengo la kuenzi kazi za Baba
wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Jambo Squared wanatarajiwa kutumbuiza katika
tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kufanyika October 14 katika
viwanja vya General trye mkoani Arusha.
Akizungumza
na vyombo vya habari moja kati ya waandaji wa tamasha hilo Devid
Runyagira kutoka Tan Communication Media ambao ni wamiliki wa redio 5
Arusha alisema kuwa tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi baba wa
taifa pamoja na kazi alizokuwa akifanya hivyo kutumia fursa hiyo kukaa
pamoja na wananchi ili kudumisha umoja na mshikamano.
“Mkoa
wa arusha una watu wengi sana hivyo tunatumia siku hii maalum ambayo ni
Nyerere Day kukutana pamoja na kushiriki michezo mbalimbali ili
kudumisha umoja wetu ambao hayati Baba wa Taifa aliusisitiza”alisema
devid.
Alisema
tamasha hilo litaanza kwa maandamano ya amani kutoka katika viwanja vya
sheikh Amri Abeid Stadium majira ya saa mbili asubuhi hadi katika
viwanja hivyo ambapo pia viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuwepo akiwemo
Mkurugenzi wa shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA) Allan Kijazi.
Mbali
na wasanii hao burudani nyingine ni pamoja na ngoma za asili kutoka kwa
Watoto wa Simba na African Culture na michezo mingine mingi ikiwemo ya
watoto.
Kwa
upande wake Vicky Mwakoyo alisema kuwa wasanii wachanga ambao
hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao watapata fursa ya kufanya
hivyo siku hiyo na zawadi mbalimbali zitatolewa kwawashindi ambao
watatangazwa katika michezo mbalimbali.
Mwakoyo
alisema kuwa kiingilio ni bure kwa watakaoingia mapema kwa maandamnao
baada ya hapo watoto watalipa shilingi 500 na watu wazima shilingi 1000
ambayo itatumika kufanya usafi uwanjani hapo.
Wadhamini wa tamasha hilo ni Kibo Palace Hotel,Pepsi,KK security,Radio 5,Shed and Sons,Shining Stars,DSTV na Trinity.
0 comments:
Post a Comment