Nafasi Ya Matangazo

November 02, 2011

KATIKA kuhakikisha inafurahia vema Siku Kuu ya Idd El Hadji na mashabiki wake, bendi ya  Extra Bongo  wana Next Level au ukipenda unaweza kuwaita ‘Wazee wa Kizigo’, watatoa burudani ya nguvu katika ukumbi wa Vatican Hotel uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Shoo ya nguvu ya bendi hiyo itatolewa katika ukumbi huo ikiwa ni baada ya kumalizika kwa shoo ya bonanza la kila Jumapili katika uwanja wa TP uliopo Sinza darajani ambapo Extra Bongo sambamba na Bantu Group hutoa burudani katika viwanja hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shoo hiyo, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani nzuri na kufurahia Siku kuu hiyo ya Idd kutoka kwa bendi yao ya Extra Bongo.

“Tumepania kuwapa raha mashabiki wetu watakaofika Vatican, tunajua wengi wao watakuwa ni watu wazima, ndio sababu tumeamua ingawa ni Siku Kuu tungeweza kufanya shoo ya kiingilio tangu mchana, sisi tutatoa burudani bure pale viwanja vya TP Sinza ili watoto nao wapate raha na kuifurahia siku kuu hii.

“Lakini kwa watakaokuja ukumbini, basi watafurahia Idd kwani tutatoa shoo kali tunazotamba nazo sasa kama ile ya Mdudu, Kizigo, Vuvuzela na nyingine nyingi kwani Super Nyamwela ambaye ni kiongozi wa shoo katika bendi amepania mno kuonyesha mavituuuz siku hiyo sambamba na wanenguaji kama Aisha Madinda, Otilia na wengine, hivyo hii si ya kukosa njoo ujioneee mwenyewe,” alisema Chocky.

Hata hivyo Chocky alisema katika kuhakikisha Siku Kuu hiyo inanoga, wameandaa kufanya shoo sambamba na kundi zima la khanga moja ama baikoko ambao bado wanaendelea na mzungumzo nao hivyo kudai kuwa shoo hiyo itakuwa ni ya kufa mtu.
Posted by MROKI On Wednesday, November 02, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo