1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akishiriki Mkutano wa
Kumi na Saba wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na
Kuenea kwa Hali ya Jangwa na na Ukame (UNCCD COP 17) unaofanyika katika Jiji la
Ulaanbaatar nchini Mongolia, Agosti 24, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula nchini Sudani Kusini Mhe, Clement Juma walipokutana katika Mkutano wa Kumi na Saba wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na na Ukame (UNCCD COP 17) unaofanyika katika Jiji la Ulaanbaatar nchini Mongolia, Agosti 24, 2026.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akishiriki Mkutano wa Kumi na Saba wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na na Ukame (UNCCD COP 17) unaofanyika katika Jiji la Ulaanbaatar nchini Mongolia, Agosti 24, 2026.
*****************
Na, Mwandishi Wetu, Ulaanbaatar, MongoliaTanzania inashiriki Mkutano wa Kumi na Saba wa Nchi
Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya
Jangwa na Ukame (UNCCD COP 17) unaofanyika katika Jiji la Ulaanbaatar nchini
Mongolia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiambata na Ujumbe wa Tanzania
wameshiriki Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Mongolia Mhe. Khurelsukh
Ukhnaa, Agosti 24, 2026.
Mhe. Masauni amesema Mkutano huo umeweka msisitizo
kupitia kaulimbiu yake ya “Ongoa Ardhi, Ongoa Matumaini”, kaliuambiu ambayo inasisitiza
kuongeza uwekezaji katika urejeshaji wa ardhi, ustahimilivu dhidi ya kuenea kwa
hali ya jangwa, ukame na usimamizi endelevu wa maeneo ya malisho.
Aidha, Mwaka 2026 pia umetangazwa kuwa Mwaka wa Wafugaji
na nyanda za Malisho jambo linalofanya ajenda ya Tanzania kuhusu uhifadhi wa
malisho na ustawi wa wafugaji kuwa muhimu zaidi katika mkutano huu.
“Kwa Tanzania, changamoto ya uharibifu wa ardhi
inahusishwa na sababu mbalimbali, zikiwemo ukataji na uharibifu wa misitu,
upanuzi wa mashamba kwaajili ya kilimo, uchomaji moto usiodhibitiwa, mmomonyoko
wa udongo, matumizi yasiyo endelevu ya ardhi na uendelezaji wa makazi.”
“Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huu unatoa fursa ya
kupata uzoefu, teknolojia, ushirikiano na rasilimali za kifedha kwa ajili ya
kuimarisha usimamizi endelevu wa malisho, urejeshaji wa ardhi iliyoharibika,
uhifadhi wa misitu, vyanzo vya maji na bioanuwai, pamoja na kuongeza
ustahimilivu wa jamii za wakulima na wafugaji katika kupambana na kuenea kwa
hali ya Jangwa na Ukame.” Amesema Mhe. Masauni.
Kwa upande wake, Afisa Kiungo wa Mkataba huo kutoka
Tanzania Bw. Thimoth Mande amesema Ushirikiano huu unawezesha Tanzania
kushughulikia kwa pamoja changamoto za uharibifu wa ardhi, upotevu wa bioanuwai
na mabadiliko ya tabianchi, badala ya kuzishughulikia kama changamoto
zinazojitegemea.
Amesema, ushiriki wa Tanzania si wa kuhudhuria mkutano
pekee, bali ni fursa ya kuonesha hatua ambazo tayari Tanzania inachukua katika
kupambana na changamoto hii, huku ikiomba kuongezewa uwekezaji na teknolojia.
Tanzania inaweza kutumia matokeo ya mkutano huu
kuhamasisha rasilimali zaidi kutoka katika mifuko ya kifedha za mazingira kama
vile GEF, IFAD, UNDP, FAO, UNEP, sekta binafsi na mifumo bunifu ya fedha, ili
kuongeza miradi hii kutoka kiwango cha maeneo maalum kwenda maeneo makubwa
zaidi.
Naye, Meneja wa Kanda ya Mashariki Kusini, Baraza la Taifa la Hifadhi
na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bi. Aminata Kirama
amesema Baraza hilo linalowajibu wa kufanya kupitia maeneo ambayo yamebainishwa
hasa katika kufanya tafiti.



.jpg)

.jpg)



0 comments:
Post a Comment