Nafasi Ya Matangazo

August 27, 2026


Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) inatoa mafunzo kwa Wachunguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu yanayofanyika katika Jengo la Mkemia, Dar es Salaam, kuanzia tarehe 26–28 Agosti 2026.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa, weledi na umahiri wa wachunguzi katika utekelezaji wa majukumu ya uchunguzi wa Vinasaba vya Binadamu, kwa kuzingatia sheria, kanuni, viwango vya kitaalamu, maadili na usiri wa taarifa za vinasaba.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias, amesisitiza umuhimu wa mafunzo endelevu katika kuhakikisha uchunguzi wa vinasaba unafanyika kwa usahihi, uadilifu na viwango vinavyokubalika, huku haki na usiri wa taarifa za wahusika vikilindwa.







Posted by MROKI On Thursday, August 27, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo