Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Waziri
Salum amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na
Uwekezaji kutoka nchini Oman Mhe.
Ibtisam Al Farooji na ujumbe wake wenye lengo la kudumisha ushirikiano wa
kiuchuni na kibiashara kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Waziri aliueleza ujumbe wa Katibu Mkuu huyo juu ya
fursa za biashara zilizoko hapa Nchini
na nia ya Tanzania kuongeza mauzo ya
bidhaa zake Nchini Oman hususani kwenye soko la mifugo na bidhaa za kilimo
Alisema mauzo ya biashara kati Tanzania na Oman yameongezeka
kutoka dola milioni 18 mwaka 2017 hadi kufikia dola milioni 160.8 mwaka 2025
huku Tanzania ikiagiza bidhaa za mafuta na gesi kutoka nchini Oman.
Tanzania na Oman zimekuwa na ushirikiano mkubwa wa
kibiashara wenye kubeba historia ya muda mrefu.




.jpeg)


.jpeg)



0 comments:
Post a Comment