Nafasi Ya Matangazo

June 16, 2026

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza  kutoa elimu na huduma za Sekta za Wizara hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yameanza  leo  Juni 16, 2026 katika eneo la Chinangali Park jijini Dodoma

Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni usajili wa wasanii na vikundi vya Sanaa, Udahili wa Wanafunzi kwenye chuo cha Maendeleo ya michezo Malya, kudahili Wanafunzi kwenye chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) kusajili Waandishi wa Habari kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Vile vile, Baraza la Michezo la Taifa linatoa elimu na kusajili vyama mbalimbali vya michezo.

Aidha, Michezo ya kitamaduni kama vile bao, drafti na karata ni michezo ambayo ni kivutio kikubwa katika banda hilo.

Ndani ya Banda hilo la Wizara ya Habari zipo taasisi zake zote ikiwa ni pamona na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Baraza la michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA),Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) 










Posted by MROKI On Tuesday, June 16, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo