Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Mkomi akizungumza na
Maafisa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la
Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo
jijini Dodoma.
Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima uwiano wa urefu kwa uzito Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Mkomi alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Daud Gwilenza akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
************
Na Mwandishi Maalumu - DodomaTaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafikisha Kampeni ya Jua Namba Zako kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kupitia maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyoanza leo katika Viwanja vya Chinangali Park vilivyopo jijini Dodoma.
Katika maonesho hayo wataalamu wa JKCI wanatoa elimu ya umuhimu wa kupima na kufahamu shinikizo la juu la damu, mapigo ya moyo, wingi wa sukari kwenye damu, uwiano wa uzito kwa urefu pamoja na wingi wa mafuta kwenye damu.
Sambamba na elimu hiyo wananchi wanaotembelea katika banda la JKCI wanapata fursa ya kuyafahamu magonjwa ya moyo, namna ya kujikinga na magonjwa yaho lakini pia kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa kupimwa vipimo vya moyo, shinikizo la damu, sukari kwenye damu pamoja na uwiano wa urefu kwa uzito.






0 comments:
Post a Comment