Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, amewataka wachimbaji wa dhahabu kuzingatia usimamizi na matumizi salama ya Kemikali ili kuepukana na madhara ya kemikali yanayoweza kuathiri afya za wananchi na mazingira.
Mkuu wa Wilaya, Tukai amesema hayo Juni 12, 2026 wakati akifungua mafunzo ya usimamizi na matumizi salama ya Kemikali kwa wachimbaji wadogo wa Nzega na tabora yaliyoandaliwa na Ofisi ya Kanda ya Kati ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika wilayani Nzega Mkoa wa Tabora.
“Inaumiza sana kupoteza nguvu kazi kwa uzembe wa kutozingatia mafunzo haya, Afya ni mtaji namba moja, tufanye uchimbaji tutumie kemikali kwa kuzingatia yale tunayoelekezwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili tuweze kulinda afya za watu na mazingira” alisema Tukai.
Naye Meneja wa Kanda ya Kati ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Magdalena Mtenga, amesema Mamlaka inahakikisha inawawezesha wananchi kwenye shughuli zao wakiwa salama kiafya pamoja na Mazingira yao kwa kuhakikisha taratibu na kanuni za matumizi salama ya kemikali yanazingatiwa.
“Mamlaka imekuwa rafiki na taasisi wezeshi kwa wananchi ili kufanikisha shughuli zao huku wakiwa salama na kuayaacha mazingira yakiwa salama, Kemikali ni muhimu zinatusaidia kuingiza kipato binafsi na pato la Taifa lakini lazima tuzingatia usimamizi na matumizi salama ya hizo Kemikali ili zisilete madhara” alisema Mtenga.
Aidha, Wadau wa Kemikali wameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwekeza katika teknolojia ikiwemo mfumo wa wa usajili wa wadau wa kemikali kwani mfumo huo umekuwa mkombozi mkubwa kwao kwenye shughuli mbalimbali za usajili na upatikanaji wa vibali vya Kemikali.
“Mfumo wa usajili wa wateja wa kemikali umerahisisha sana kazi na kuokoa muda na fedha, kwa sababu huhitaji kwenda ofisini, bali kwa njia ya mtandao tu unaweka nyaraka















0 comments:
Post a Comment