Nafasi Ya Matangazo

June 04, 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amesema suala la uhifadhi wa mazingira ni mtambuka linahitaji ushirikiano wa sekta zote.
 
Amesema hayo wakati akizungumzia katika kipindi cha ‘Kumekucha’ kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV leo Juni 04, 2026 jijini Dodoma ambapo alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia sekta hiyo ili ilete maendeleo endelevu.
 
Mhe. Kwagilwa alieleza kuwa kwa kutambua umuhimu huo Serikali imelipambanua suala la mazingira na mabadiliko ya tabianchi kuwa ni mojawapo ya nguzo tatu zilizopo kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
 
“Tunatambua shughulI zote za kiuchumi zinafanyika kwenye mazingira yetu hivyo tunao wajibu wa kuyatunza kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwani inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 idadi ya Watanzania itakuwa watu milioni 118 mara mbili ya idadi ya sasa hivyo shughuli zinazoathiri mazingira zitakuwa nyingi Zaidi,” alisema.
 
Mhe. Kwagilwa alifafanua kuwa katika miaka ijayo uchumi utakua na kwamba sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, uchimbaji wa madini zitaathiri mazingira hivyo lazima kama nchi iwe na mkakati madhubuti wa kuhakikisha kuwa mazingira yanahifadhiwa bila kuwathiriwa.
 
Aidha, akizungumzia Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea hapa nchini, alisema kuwa pamoja na mambo mbalimbali Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa maonesho yanayohusisha takriban taasisi za Serikali zisizo za Serikali takriban 80.
 
Alisema maonesho hayo ni katika kuhakikisha Serikali inaweka jitihada madhubuti za kusimamia mazingira kwa kuwashirikisha na kuwakaribisha wadau mbalimbali kuonesha na kutoa elimu ya ubunifu na teknolojia ya usimamizi wa taka.
 
“Tukiwa katika wiki hii ya kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira Duniani tunayo mabanda ya wadau wanaoonesha namna ya kuchakata taka, kuzirejeleza au kuzitumia tena, wananchi wanapata elimu hatua itakayosaidia kupunguza taka zinazozogaa na kuchangia uzalushaii wa gesijoto,” alisema.
 
Kwa upande mwingine Naibu Waziri hiyo alisema Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) likiwa Mamlaka kamili itaweza kutekeleza majukumu kwa nguvu zote bila uonevu
 
Alisema hivi sasa kuna sheria mbalimbali zenye mnasaba na mazingira lakini ziko kwenye sekta tofauti tofauti zikiwemo ya Maji, Usafi na Usafi na Mazingira ambazo NEMC haina meno ya kuziingilia hivyo, ikiwe Mamlaka kamili itakuwa na nguvu ya kuwawajibisha wanaokiuka sheria.
 
 
 
Posted by MROKI On Thursday, June 04, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo