Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa
Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN
University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla
iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026. Rais Mhe.
Dkt. Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu kutokana na mchango wake katika
Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania,
pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo
kupitia sekta ya Utalii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi wa Chuo Kikuu cha
Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Wanafunzi wa Chuo hicho, wageni
mbalimbali baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa)
kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni,
2026. Viongozi wa Chuo Kikuu cha
Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Wanafunzi wa Chuo hicho pamoja na
wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa
Heshima (Honoris Causa) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan, Chuoni hapo Moscow nchini Urusi tarehe 04 Juni, 2026.



















0 comments:
Post a Comment