Waziri wa Inchi Ofisiya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Kikwete ametoa pongezi hizo leo Juni 17/2026 Jijini Dodoma alipotembelea banda la TEA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini hapa.
Katika maonesho hayo Kikwete alikuwa mgeni rasmi wa maonesho hayo ambapo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya taasisi mbali mbali za hapa nchini.
Akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na TEA Afisa uhusiano na mawasiliano wa Mamlaka hiyo Eliafile Solla amesema taasisi hiyo inatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake, huduma mbalimbali zinazotolewa pamoja na miradi mbalimbali inayotelekezwa kwa fedha za mfuko wa Elimu wa Taifa.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 yalianza Juni 16 na ynatarajiankumalizika Juni 23 mwaka huu.







0 comments:
Post a Comment