Nafasi Ya Matangazo

April 23, 2026










Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Imeelezwa kwamba Serikali kupitia Wizara ya Madini na Taasisi zake itaendelea kuwawezesha kwa kuwajengea uwezo  wanawake, vijana na watu wenye uhitaji maalum kwa kuwapatia  vifaa vya uchimbaji , mitambo ya uchorongaji miamba na kuwapatia maeneo ya leseni yaliyofanyiwa utafiti wa kina ili kuwaendeleza na uchimbaji bora na wenye tija bila kupoteza mitaji na muda.

Rai hiyo imetolewa leo Aprili 23, 2026 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akikabidhi  Pampu 10 za kutolea maji mgodini kwa Chama cha Wanawake wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) kwenye Kongamano la fursa na mageuzi kwa wanawake katika  sekta ya madini nchini liliofanyika jijini Dodoma.

Waziri Mavunde amesema kwamba, kupitia Program wezeshi ya _Mining For A Brighter Tommorrow_ (MBT), itaendelea kuwawezesha wanakimama na vijana kwa kuwapatia leseni  zilizofanyiwa utafiti wa kina wa jiosayansi na mitambo ya kusaga mawe ili kuendelea kuwawezesha kuchimba kwa tija na uhakika.

Waziri Mavunde amesema kuwa, mpaka sasa wachimbaji wadogo wanachangia asilimia 40 katika makusanyo kwenye sekta ya madini ambayo ni mpaka mwezi April trilioni 1.1 

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt.Venance Mwase amesema , STAMICO itaendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo katika makundi yote kwa kuwapatia mashine , 
kuwafanyia utafiti  lengo ni kufikia Dira ya 2030  inayosema Madini ni Maisha na Utajiri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAWOMA Bi.Semeni Malale ameeleza kuwa kupitia mradi wa kimkakati wa Malkia wa Madini unaendelea kuwaunganisha wanawake na vijana nchini kwa kufungua fursa za uwezeshaji katika mikoa mbalimbali hususan katika suluhisho la kuongeza tija na kipato.

Malale ameongeza kuwa 
mpaka sasa mradi wa malkia wa madini umefanikiwa kuwaendeleza  kiuchumi wanawake 7000 katika mikoa 21 na vijana 120.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri akimwakilisha Mkuu wa Mkoa ameipongeza  TAWOMA kwa kuwaingiza vijana wengi katika mnyororo wa thamani madini ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ilionyesha idadi ya vijana katika taifa  kuwa na  asilimia 21 ya wakazi wote.

Washiriki wengine katika kongamano hilo ni pamoja na Tume ya Madini,Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Benki ya CRDB, Azani , GF Truck.
Posted by MROKI On Thursday, April 23, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo