Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha-Rose Migiro, anaondoka nchini leo kuelekea Beijing, Jamhuri ya Watu wa China, kwa ziara ya kikazi ya siku sita kufuatia mwaliko wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Ziara hiyo inalenga kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama cha Kikomunisti cha China.
Ziara hii inafanyika katika kipindi ambacho mwaka 2026 umetangazwa rasmi kuwa mwaka wa kukuza uhusiano na maelewano ya kijamii na kitamaduni kati ya China na Afrika. Hivyo, mwaka huu unatoa fursa adhimu ya kuimarisha urafiki, kubadilishana uzoefu na kujenga uelewano wa pamoja kati ya vyama hivi viwili.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu ataambatana na ujumbe wa watu watano.
Akiwa nchini humo, yeye pamoja na ujumbe wake watafanya mazungumzo na viongozi wa juu wa Chama cha Kikomunisti cha China.







0 comments:
Post a Comment