Nafasi Ya Matangazo

March 16, 2026



Bukombe , Geita
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameonyesha kuridhishwa na kushangazwa na kasi ya teknolojia inayotumika katika Kituo cha Mfano cha Uchenjuaji Dhahabu cha Katente, kilichopo wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa leo Machi 15 , 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Subira Mgalu  wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya kituo cha mfano cha Katente kilichoanzishwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kikilenga kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini katika uchenjuaji bora  ili kuachana na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki.

Mgalu ameeleza kuwa , kamati imefurahishwa na  teknolojia ya uchenjuaji dhahabu  inayotumika Katente, inatumia mifumo ya kisasa ya Vat Leaching, imefanikiwa  kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kutoka asilimia 40 hadi kufikia zaidi ya asilimia 90.

Pia, ameipongeza STAMICO kwa kurahisisha upatikanaji wa kemikali , na vilipuzi huduma nyingine zinazoendana na uchimbaji mdogo kwa wachimbaji wadogo wapatao 1019 kupitia  kituo cha mfano.

Sambamba na hapo, Mgalu ameipongeza Serikali kwa kusogeza huduma kwa wachimbaji wadogo kupitia  kituo cha Katente, hatua hii inawasaidia wachimbaji wadogo katika kuongeza   tija  kwenye shughuli zao za uchimbaji.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri mzuri kuhusu kuboresha kituo cha mfano ili kuendana na idadi ya wachimbaji wadogo katika kuwapatia huduma.

Awali , akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za uchenjuaji  katika kituo cha mfano cha Katente, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO  Deusdedith Magala  amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi Januari 2026 wachimbaji wadogo wapatao 1920  wamepata elimu juu uchimbaji , usagaji mbale, uchenjuaji na ukamatishaji dhahabu.
Posted by MROKI On Monday, March 16, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo