Nafasi Ya Matangazo

February 25, 2026


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Feb 25,2026 amekutana na Gavana wa Jimbo la Maniema-Congo DRC Mhe Mussa Kabwankubi Moise akiwa ameambatana na ujumbe wake alipomtembelea Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao wamekubaliana mashirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi na Masuala ya Kiusalama kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Jimbo la Maniema.

Aidha RC Chalamila amesema Congo na Tanzania ni majirani na ni marafiki wa muda mrefu ndiyo maana katika Mkoa wa Dar es Salaam wakongo ni wengi na wanajishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo biashara

"Ukiangalia  kupitia Bandari ya Dar es Salaam mzigo unaokwenda Congo kitakwimu ni kiasi kikubwa kwa mwaka hivyo Mkoa unathamini sana wacongo" Alisema Chalamila










Posted by MROKI On Wednesday, February 25, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo