Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa sekta ya mafuta nchini ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha, salama na yanayopatikana kwa bei shindani kwa manufaa ya Taifa
.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Januari 31, 2026 jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wawekezaji wa Kampuni za Mafuta nchini.
Mramba amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wa mafuta ya petroli na dizeli pamoja na kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji, hatua itakayosaidia kuhakikisha uhakika wa mafuta nchini.
Aidha, aliwashukuru wadau wa sekta hiyo kwa ushirikiano wao mzuri na Serikali, hususan katika kipindi cha uchaguzi, hali iliyosaidia kudumisha utulivu na upatikanaji wa mafuta nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, Kamishna wa Petroli na Gesi, Bw. Godluck Shirima, pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.










0 comments:
Post a Comment