Nafasi Ya Matangazo

October 15, 2025

PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo Oktoba 15,2025 katika kata ya Puma wilaya ya Ikungi ndani ya Jimbo la Ikungi Magharibi  mkoani Singida.

Akiwa Katika mkutano huo,Dkt.
Nchimbi aliinadi Sera na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025-2030 kwa Wananchi ikiwemo na kuwaomba  kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Aidha,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo  kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ikungi Magharibi Ndugu Elibariki Immanuel Kingu,mgombea Ubunge jimbo la Ikungi Mashariki Ndugu Thomas Mgonto KITIMA na Madiwani.

Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 23 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.








NCHIMBI AENDELEA KUCHANJA MBUGA AKISAKA KURA ZA CCM SINGIDA VIJIJINI.

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi  ameendelea kuchanja mbuga kwa ajili ya kuomba kura za mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Leo Oktoba 14,2029 Dk.Nchimbi anafikia mkoa wa 23, akifanya mkutano mkubwa wa kampeni katika Uwanja wa CCM uliopo Kata ya Ilongero, jimbo la Ilongero katika Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.

Akiwa katika mkutano huo Dkt.Nchimbi ameendelea kumuombea kura Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili ashinde kwa kishindo, kuomba kura za wabunge na madiwani.

Mbali ya kuomba kura za wagombea wa CCM, pia akiwa katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jimbo hilo pia ametumia nafasi hiyo kunadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030.

Wakati huo huo Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ilongero, Ndugu Haidary Gulamali na Madiwani.



Posted by MROKI On Wednesday, October 15, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo