Nafasi Ya Matangazo

June 04, 2025



Imeelezwa kuwa, mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku katika maeneo ya vijijini na pembezoni imelenga kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 
  
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masinde mara baada ya kupokea taarifa ya miradi ya usambazaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuwasilishwa na Mhandisi wa Miradi wa REA, Bi. Annet Ndyanabo mkoani Shinyanga. 

Mhe. Masinde ameeleza kuwa, miradi ya nishati safi itapunguza ukataji wa miti unaosababisha mabadiliko ya tabianchi pamoja na vifo vinavyosababishwa na kuvuta hewa chafu inayotokana na kuni na mkaa.
Posted by MROKI On Wednesday, June 04, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo