Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mheshimiwa Stanslaus Nyongo (Mb.), akichangia hoja Bungeni jijini Dodoma leo, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2025/26. Mjadala ulihitimishwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo,
amehitimisha mjadala wa wabunge kuhusu hali ya uchumi na Mpango wa Maendeleo wa
Taifa kwa mwaka 2025/2026, akisisitiza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa
imara na himilivu katikati ya mdororo wa uchumi duniani
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo, Prof. Mkumbo alitumia takwimu za ukuaji
wa Pato la Taifa (GDP) na Mfumuko wa Bei kuonesha kuwa Tanzania inafanya vizuri
ikilinganishwa na wastani wa kimataifa na hata kikanda
Akifafanua zaidi, Waziri Mkumbo alieleza kuwa wakati dunia na kanda
zikikabiliwa na changamoto za kiuchumi, Tanzania imefanikiwa kudhibiti mfumuko
wa bei, ambao ulikuwa asilimia 3.1 mwaka 2024,the kiwango ambacho ni
chini sana ya wastani wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) cha
asilimia 54.6 na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) cha asilimia 23.
Aidha, alibainisha kuwa Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 5.1 mwaka 2023 na
linakadiriwa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2024, viwango ambavyo ni vya juu
kuliko wastani wa dunia (3.3%) na nchi za SADC (3.1%)
"Alisema siri ya ustahimilivu huu ni mseto wa vyanzo vya uchumi, vikiwemo
kilimo, utalii, madini, na ujenzi"
Prof. Mkumbo aliorodhesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha
miaka minne ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo yamechangiwa na
bajeti zilizopitishwa na Bunge
Alitaja uwekezaji mkubwa katika huduma za jamii, ikiwemo matumizi ya Shilingi
trioni 1.3 kwa ajili ya elimu bila ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha
sita, na Shilingi trioni 2.7 zilizotolewa kama mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu.
Pia aligusia mpango wa Serikali wa kutekeleza Bima ya Afya kwa Wote, ambao
umewekewa vyanzo vya mapato katika bajeti ya mwaka huu
Akiwajibu wale wanaokosoa na kutoona mafanikio yaliyofikiwa, Waziri Mkumbo
alirejelea maneno ya Rais wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi, aliyewahi
kusema, "...asiyeyaona maendeleo kwa sababu macho ni magonjwa atege
masikio asikilize haya tunayoyasema!"
Alisema ni muhimu kwa wananchi kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya
CCM.
Katika hotuba yake, Waziri alikiri kuwa maendeleo ni mchakato endelevu wenye
mafanikio na changamoto, akitolea mfano wa Mwalimu Nyerere ambaye alikiri na
kusahihisha baadhi ya makosa yake ya kisera.
Alimsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kiongozi mwenye ujasiri wa
kuendeleza mema, kusahihisha yaliyokosewa, na kukabiliana na changamoto Mjadala
wa mpango huo ulihitimishwa baada ya wabunge 97 kutoa michango yao.
Prof. Mkumbo alitoa shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na
kumpongeza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa kuwasilisha bajeti
iliyopokelewa vizuri na wananchi na vyombo vya habari.
Alihitimisha kwa kuwataka wabunge kwenda majimboni kuwaombea kura Rais Samia
Suluhu Hassan na chama cha CCM katika uchaguzi ujao.
0 comments:
Post a Comment