Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2025

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mweka Hazina wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania, Abdilah Omar  (wa tatu kushoto) alipotembelea mabanda ya maonesho akimwakiliasha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya  Uelewa kuhusu Ualbino Kwenye uwanja wa Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania, Godson Mollel.   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya World Share, Bw. Worm Ann (wa pili kushoto) alipotembelea banda la maonesho la taasisi hiyo akimwakiliasha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya  Uelewa kuhusu Ualbino kwenye uwanja wa Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete na kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, Dr. Diwani Msemo alipotembelea banda la maonesho la taasisi hiyo  akimwakiliasha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siiku ya Kimataifa ya  Uelewa kuhusu Ualbino kwenye uwanja wa Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025.  Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania, Godson Mollel. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mratibu wa Afya wa Taasisi ya Standing Voice, Christina Silas (kulia) aliyetoa maelezo kuhusu kofia na vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na watu wenye ualbino kujikinga na athari za jua alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimaatifa ya  Ulewa kuhusu Ualbino kwenye uwanja wa  Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025.  Wa tatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete,  wa pili kushoto  ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania, Godson Mollel. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya World Share, Bw. Worm Ann ( kushoto) alipotembelea banda la maonesho la taasisi hiyo akimwakiliasha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya  Ulewa kuhusu Ualbino kwenye uwanja wa Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025.  Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete na kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maandamano alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya  Ulewa kuhusu Ualbino kwenye  uwanja wa Mwanga Centrę Mjini Kigoma, Juni 13, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunusi, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobia Andengenye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, Mwenyenyekiti wa Chama cha Wenye Ualbino Tanzania, Godson Mollel na. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoka wa Kigoma, Jamal Tamim. 

**************

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawathamini Watu wenye Ulemavu wakiwemo wenye ualbino na wakati wote itahakikisha inawalinda na kuwapatia fursa stahiki katika ujenzi wa Taifa.

 

Amesema katika kuendelea kutekeleza mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutumia mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, hadi kufikia Machi, 2025 tayari shilingi bilioni 5.48 zimetolewa kwa vikundi 891 vya Watu Wenye Ulemavu nchini.

 

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mahsusi za kuimarisha ustawi na utoaji huduma kwa watu wenye ualbino ikiwemo kuwatambua, kuimarisha mifumo ya kisera na kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu hapa nchini.

 

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa (Juni 13, 2025) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino yaliyofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre, mkoani Kigoma.

 

Ameongeza kuwa katika mwaka 2024/2025 kiasi cha ruzuku inayotolewa kwa Vyama vya Watu wenye Ulemavu kimeongezeka hadi kufikia shilingi milioni 230 ikilinganishwa na shilingi milioni 200 zilizotolewa kwa mwaka 2023/2024.

 

Akizungumza kuhusu kuimarika kwa utoaji wa huduma za afya kwa watu wenye Ualbino, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Juni 2024 Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ilitumia zaidi ya shilingi milioni 500 kusambaza katika mikoa yote 26 ya Tanzania mafuta kinga ya saratani ya ngozi kwa Watu wenye Ualbino. 

 

“Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali ilitenga shilingi bilioni 8.743 kwa ajili ya huduma za ustawi wa Jamii na shilingi 182. 8 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta kinga ya saratani ya ngozi kwa watu wenye Ualbino”.

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa wahakikishe wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu wenye Ualbino, Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Taarifa za Watu wenye Ulemavu (PD-MIS) katika ngazi ya Halmashauri.

 

Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kupitia maadhimisho hayo, Serikali imezindua programu janja ‘Albino Mobile App’ ambayo itawezesha kufanya usajili na ukusanyaji wa taarifa za watu wenye ualbino kwa njia ya kidigitali.

 

Amesema kuwa mfumo huo utarahisisha, utaharakisha na utahakikisha usahihi katika usajili wa watu wenye ualbino na ulemavu nchini Tanzania, hususan walioko maeneo ya pembezoni. “Mfumo huu utapunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa vifaa kwa ajili ya usajili, na pia kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi zinazosaidia Serikali kupanga na kutekeleza sera kwa ufanisi”

 

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) Godson Mollel Amesema kuwa Serikali imefanya mambo makubwa yenye lengo la kuwawezesha watu wenye Albino nchini ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya kununua mafuta kinga ambayo hugawiwa bure.

 

“Pia, Serikali imetoa agizo kwa halmashauri kutoa fedha kwa ajili ya kununua mafuta kinga ambayo imesaidia kupunguza uhaba wa mafuta kinga”

 

Pia, Godson amewataka watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 2025 “Jitokezeni kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu, mkifanya hivyo mtakuwa mmetimiza haki yenu ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa”

 

Katika Maadhisho hayo Mheshimiwa Majaliwa alizundua Programu janja ya usajili ya wenye ualbino ‘Albino Mobile App’. itakayowezesha kuwasajili na kuwatambua wenye ualbino.


Posted by MROKI On Friday, June 13, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo