Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya
uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:-
i. Jaji Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma, ameteuliwa kuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Mheshimiwa Prof. Juma anachukua
nafasi ya Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax ambaye ni Waziri wa Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa; na
ii. Dkt. Deo Mwapinga ameteuliwa kuwa Balozi. Dkt. Mwapinga ni Katibu Mkuu wa
Jukwaa la Wabunge wa Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda
wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR).
0 comments:
Post a Comment