Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akizungumza na wanachi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Bahi alipotembelea Halmashauri ya Wilaya
ya Bahi mkoani Dodoma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akiweka jiwe la msingi ujenzi wa
Shule ya Sekondari ya Amali katika Kijiji cha Nzali, Wilaya ya Chamwino mkoani
Dodoma akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
2020-2025 mkoani humo.
************
Na Mwandishi Wetu, Chamwino
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),
kimewashukuru na kuwapongeza viongozi wa dini kwa ushauri kuhakikisha mchi
inaendelea kuwa na amani hususan kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na
kubariki uchaguzi huo uendelee huku, ikisisitiza kuwa haidharau maoni
yanayotolewa.
CCM imesisitiza kuwa haipuuzi
ushauri mbalimbali unaotolewa kuelekea uchaguzi huo, lakini imesisitiza
hautaahirishwa kwa kuwa mageuzi na mabadiliko ni jambo endelevu na haiwezi kuwa
hoja ya kuahirisha uchaguzi.
Hayo yalielezwa jana Chamwino
mkoani Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akipokea taarifa ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 akiwa katika siku ya kwanza
ya ziara yake mkoani humo.
"Uchaguzi utaendelea sio
kwamba tunapuuza mawazo, tutaendelea kuzungumza mambo ambayo yanaendelea, na
tunashukuru sana nchi imetulia. Viongozi wetu wa kiroho wametuongoza wametupa
ushauri mzuri sana na mimi nashukuru sana kwa kututia moyo na kutuambia
uchaguzi uendelee lakini kwa amani," alisema.
Wasira alisema CCM ni Chama
kinachozungumza na kuhimiza amani ndio maana taifa limekuwa na utulivu kwa
miaka 60, alisisitiza kwamba hilo linafanya Chama kijivunie kwa kuwa ni
ushahidi kwamba kinaweza kusimamia amani.
Alisisitiza haki iko ndani ya
amani na kwamba ukiondoa amani utavunja haki za watu wengi hususan wanyonge,
"ukiondoa amani watakaoumia hasa ni wanawake, watoto na walemavu."
"Amani ni lazima sasa
kuna wanaosema haki, na sisi tunasema ndani ya amani kuna haki, na haki hiyo
inalindwa na amani kwa sababu ukiiondoa watu wengi wataathirika wala sio mtu
mmoja ni wengi sana na ushahidi wake upo, sisi tumepokea wakimbizi maelfu
kutokana na kuvunjia kwa amani kwa majirani zetu," alisisitiza.
MKAKATI KUIMARISHA UCHUMI
Akizungumzia kuhusu Akilimo na
uzalishaji wa chakula Wasira alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ijayo, pqmoja na
mambo mengine itatilia mkazo zaidi uzalishaji hususqn kwa wananchi walioko
vijijini kupambana na umasikini.
"Umaskini unaweza
kuondoshwa kama unawasaidia watu wa vijijini wapate njia bora ya uwekezaji,
Progaramu ya Jenga Kesho Bora (BBT) ikiwa 'transformed' (ikiboreshwa) kaenda
kila mkoa na wanakijiji sio tu kwa vijana wasomi itabadilisha maisha.
"Umwagiliaji ni lazima
usambazwe na kwa kweli ninampongeze sana Rais Samia (Dk. Samia Suluhu Hassan),
mimi nilikuwa Waziri wa Kilimo tatizo ambalo lilitukabili katika umwagiliaji ni
kutokuwa na mfumo maalumu wa usimamizi wa suala hilo, kama huna hela humwagilii,
utamwagilia na mvua tu kwa sababu miundombinu ya umwagiliani ni gharama,"
alisema.
Alieleza kwa mfano Vietnam ni
wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo kuliko nchi yoyote, "ukiweka
'iregation' Dodoma italeta mabadiliko kwa sababu mvua za hapa hazitabiriki."
"Sasa mkifanya
umwagiliaji kitu kinaichoitwa njaa na umasikini vitaisha, kwa hiyo uangaliwe
uwezekano wa kutumia maji ya mvua kutengeneza mabwawa ya kufanya umwagiliaji
ili watu inapowezekana walime kwa kutumia trekta badala ya jembe la mkono ambalo
ni shingo ya umasikini.
"Jembe la mkono kwa sasa
kwa vijana ni tatizo, na watu tusiwategemee sana kulima kwa jembe la mkoni.Hiki
kitu katika ilani inayokuja tutatazama uwezekano wa kuweka mfumo matrekata ya
kutoa huduma ili wakulima wawe wanatumia na kurudisha kwa kulipia,"
alisma.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akiwa katika moja ya vyumba vya
kutolea huduma katika Hospitali ya
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma , akiwa katika ziara kukagua
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani humo.
DK. SAMIA ANAKWENDA VIZURI
Akizungumzia kasi ya
maendeleao, Wasira alisema kwa kipindi cha miaka minne nchi chini ya Rais Dk.
Samia imszidi kupiga hatua kubwa.
"Kazi ambazo amezifanya
Rais Samia kwa miaka minne ni kubwa. Maana unauliza tumetoka wapi na tuko wapi
miaka minne baada ya kifo cha Rais Dk.
John Pombe Magufuli ambaye kaulimbiu yake ilikuwa hapa kazi tu, nchi
imeendelea kuimarika.
"Rais Samia akaja na
kaulimbiu kwamba kazi iendelee na kazi imeendelea. Reli ya SGR aliachiwa karibu
kufika Morogoro, leo hii ipo Makutupora (Singida), viipande vinavyobakia kutoka
Mwanza kimoja kipo asilia 86 kwenda Isaka na kutoka Isaka kwenda Tabora kazi
inaendelea," alisema.
0 comments:
Post a Comment