Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Neema Mbuja amesema kile ambacho wanawake walikipambania katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ya Kimataifa ili kuwa na haki, usawa na uwezeshaji kwa wanawake matunda yake yanaonekana hivi sasa.
Mbuja ameyasema hayo alipokuwa akieleza safari ya mwanamke katika kudai haki, usawa na uwezeshaji kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.
"Wanawake wengi walipambana kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia, usawa wa utendaji kazi na ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na tangu kufanyika kwa Mkutano wa Beijing mwaka 1995 mambo yote ya usawa kwa sasa yanaonekana kwa vitendo." Amesema Mbuja
Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kinara katika kuhakikisha haki kwa mwanamke inapatikana.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Nishati inajivunia kwa uwepo wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
0 comments:
Post a Comment