Mawakili wa Serikali nchini wamekumbushwa juu ya majukumu yao wakati wa kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samweli M. Maneno amezungumza hayo tarehe 27 Machi, 2025 wakati wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yanayofanyika Jijini Arusha.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa Mawakili wa Serikali, kwakuwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo, na kuwakumbusha masuala mbalimbali ya kisheria kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Mawakili wa Serikali.
*“Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza kwa kuhudhuria mafunzo haya muhimu ambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameyaandaa na kuyaratibu ili tuweze kupata Suluhu ya Umahiri.”* Amesema Mhe. Maneno
Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewasisitiza Mawakili wa Serikali kuhakikisha kwamba ushauri wa kisheria wanaoutoa kwenye taasisi zao unatekelezwa, na pindi wanapokutana na changamoto kwenye kutekeleza jukumu hilo watoe taarifa kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
*“Tunatamani Wanasheria wote waione Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndio kimbilio lao, pale wanapokutana na changamoto wakati wanapokuwa wanatoa ushauri wa kisheria.”* Amesema Mhe. Maneno
Katika hatua nyingine, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amewahakikishia Mawakili wa Serikali kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itasimama mstari wa mbele kuhakikisha nafasi ya Wanasheria hao kwenye taasisi zao inaonekana na wakati wowote milango ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iko wazi kuwapokea na kuwapa ushauri juu ya namna ya kutekeleza vyema majukumu yao.
*“Sisi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tutawasikiliza na kuwapa ushauri ili muweze kutekeleza vyema majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.”* Amesema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikal
Mafunzo kwa Mawakili ya Serikali yanayoendelea Jijini Arusha yamekuwa fursa nzuri kwa Mawakili wa Serikali kuendelea kujifunza na kuongeza ujuzi kwenye maeneo mbalimbali ya kisheria kutokana na mada zinazotolewa na wakufunzi wabobezi wa masuala ya kisheria.
0 comments:
Post a Comment