
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa mazingira katika hafla iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa mazingira la ‘The Nature Conservancy’ ya kuwashukuru wadau na kukuza mahusiano na washirika wa taasisi hiyo iliyofanyika usiku wa Machi 27, 2025 jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Nature Conservancy, Ademola Adjagbe akizungumza kuhusu umuhimu wa kushirikiana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukuza uhifadhi, katika hafla iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa mazingira la ‘The Nature Conservancy’ iliyofanyika usiku wa Machi 27,2025 jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa hafla iliyoandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa mazingira la ‘The Nature Conservancy’ ya kuwashukuru wadau na kukuza mahusiano na washirika wa taasisi hiyo iliyofanyika usiku wa Machi 27, 2025 jijini Arusha wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb)(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
************
Na Happiness Shayo-Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema kuwa jamii zimeendelea kunufaika na
biashara ya hewa ukaa kupitia miradi ya
Shirika la Uhifadhi wa mazingira la ‘The Nature Conservancy’ nchini
Tanzania lililojikita katika kuhifadhi mifumo ya ikolojia , kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza mapato kwa jamii.
Ameyasema hayo katika hafla ya
kuwashukuru wadau na kukuza mahusiano na washirika wa taasisi hiyo iliyofanyika
usiku wa Machi 27, 2025 jijini Arusha.
“Tunashukuru sana kwa msaada wa The
Nature Conservancy, hasa kwa kushirikiana na Carbon Tanzania, kuanzisha miradi
ya kaboni katika maeneo muhimu kama vile Yaeda Chini, Makame Wildlife
Management Area (WMA), Ntakata, na misitu ya Tongwe. Ushirikiano huu sio tu
unasaidia kulinda mifumo muhimu ya ikolojia lakini pia hutoa fursa muhimu kwa
jamii za wenyeji kufaidika kupitia mbinu bunifu za uhifadhi na kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi” amesema Mhe.Chana.
mefafanua kuwa kupitia biashara ya kaboni Msitu wa Ntakata ulio chini ya Serikali ya vijiji, wilaya ya Tanganyika, umeingiza dola milioni 24 katika mapato kwa jamii tangu Juni 2019 na kwamba Carbon Tanzania inaendelea kuhakikisha jamii katika vijiji 8 inapata dola milioni 12 kila mwaka (takribani tzs bilioni 3 hadi 4 kila mwaka).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Nature Conservancy, Ademola Adjagbe amesema kuwa Shirika hilo linafanya kazi katika nchi zaidi ya 80 duniani katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi wa mazingira.
Ameongeza kuwa Afrika inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimazingira zinazopelekea upotevu wa rasilimali hivyo ni vyema kushirikiana kuhakikisha Maliasili zinaokolewa, maisha ya binadamu yanalindwa, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kutunza baioanuwai.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la The Nature Conservancy’s, wadau mbalimbali wa uhifadhi kutoka Serikalini na Sekta Binafsi.
0 comments:
Post a Comment