Nafasi Ya Matangazo

February 17, 2025

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal(katikati mara baada ya kikao kuhusu namna ya kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, kilichofanyika jijini leo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal, kuhusu namna ya kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, ikiwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa nyara na mazao ya misitu, uvuvi haramu na usalama wa baharini, katika kikao kilichofanyika leo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal(hayupo pichani), kuhusu namna ya kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, ikiwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa nyara na mazao ya misitu, uvuvi haramu na usalama wa baharini, katika kikao kilichofanyikaleo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal (wa pili kutoka kushoto) akizungumza katika kikao kati yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (hayupo pichani) kilichofanyika leo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam. Wengine ni Maafisa kutoka wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal, kuhusu namna ya kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, ikiwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa nyara na mazao ya misitu, uvuvi haramu na usalama wa baharini, katika kikao kilichofanyika leo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi. Ashita Mittal(katikati), pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na UNODC mara baada ya kikao kuhusu namna ya kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, kilichofanyika jijini leo Februari 17,2025 jijini Dar es Salaam.
****************
Na Happiness Shayo-Dar es Salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), imejipanga kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kudhibiti uhalifu unaoathiri mazingira (Enviromental Crimes) na  kulinda bayoanuwai.
 
Hayo yamejiri leo Februari 17,2025 katika kikao kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) na Mwakilishi wa Kanda wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), Bi.Ashita Mittal, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana amesema kupitia kikao hicho Wizara ya Maliasili na Utalii na UNODC wamepata fursa ya kuangalia jinsi UNODC inavyounga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, ikiwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa nyara na mazao ya misitu, uvuvi haramu na usalama wa baharini.
 
Pia, Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa UNODC kwa msaada wa kifedha na kiufundi uliotolewa kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka (Transnational Organized Crimes) ikiwemo Biashara Haramu ya Nyara(IWT) kupitia Kitengo cha Udhibiti wa pamoja kilichopo Bandari ya Dar es Salaam (Joint Port Control Unit – JPCU).
“Biashara Haramu ya Wanyamapori  sio tu inaleta tishio kwa usalama wa rasilimali za wanyamapori na misitu miongoni mwa nchi wanachama, hivyo kuathiri uchumi wetu na kuwezesha uhalifu mwingine wa kupangwa kama vile utakatishaji fedha na ugaidi”Mhe. Chana amesisitiza.
 
Kwa upande wake, Bi.Ashita Mittal ameahidi kuwa UNODC itaendelea kushirikiana na  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya uhalifu unaovuka mipaka kwa kutoa zaidi mafunzo katika nyanja mbalimbali na vitendea kazi kupitia programu mbalimbali zitakazoandaliwa na pande zote mbili.
 
Kikao hicho kimehudhuriwa na Maafisa kutoka UNODC na Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Posted by MROKI On Monday, February 17, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo