Nafasi Ya Matangazo

February 27, 2025



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 27 Februari, 2025 ameongoza mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali wa serikali katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu waliofariki katika ajali tarehe 25 Februari, 2025 iliyohusisha basi la kampuni ya CRN na gari la Serikali katika eneo la Shamwengo, jijini Mbeya.

Shughuli hiyo imefanyika leo tarehe 27 Februari, 2025 katika Viwanja vya Uhindini jijini Mbeya, ambapo waliofariki katika ajali hiyo ni Daniel Mselewa, Thadeo Thadeo, Isaya Geazi na Furaha Simchima.

Katika hotuba yake, Dkt. Tulia ametoa pole kwa familia za marehemu na wote walioathirika na ajali hiyo, huku akiwataka wananchi na viongozi kuendelea kudumisha ushirikiano, umoja na mshikamano katika kipindi hiki kigumu ili kwa pamoja waendelee kujenga taifa imara.
Posted by MROKI On Thursday, February 27, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo