Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2025





Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dr. Samia Suluhu ameridhia malipo ya shilingi Milioni 800.65 kwa wananchi 429 wa Kata ya Mkange wanaopisha ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki inayojengwa toka Tanga kupita Kata hiyo hadi Makurunge Bagamoyo. 

Akizungumza katika mkutano huo na wananchi wa vijiji Vitano vya kata hiyo, Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Ndugu Ridhiwani Kikwete aliishukuru serikali kwa kuendelea kutatua kero za wananchi na kumshukuru Mh. Rais kwa kuridhia fedha hizi zilipwe ili wananchi wapishe na kupata maendeleo. Akiishukuru serikali, Mbunge ameeleza shukrani zake kwa serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya barabara mbalimbali katika halmashauri hiyo ambazo zinakwenda kuongeza tija kiuchumi kwa wananchi wanaopitiwa na miundombinu hiyo. Pia Mbunge aliishukuru serikali kwa matayarisho ya ujenzi wa barabara toka Mandera hadi Saadan ambayo inakwenda kufungua fursa kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mkutano huo wananchi wa mkange wameeleza furaha yao na kumshukuru Mbunge wao ambaye siku zote amekuwa akipambana kuhakikisha anatatua changamoto zao. Alhaj Khamis Nassor, sheikh wa Mkange alieleza kuridhishwa sana na jinsi Mbunge wao anavyoshughulika na changamoto za wananchi sio tu Mkange lakini pia Halmashauri yote ya Chalinze. 

Akizungumza kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Chama  hicho Ndg. Mwidadi Mauya ameeleza kupokea taarifa hii kwa furaha kubwa uku akinadi kuwa sasa anakwenda kukisimamia Chama bila kigugumizi kwa kuwa hili lilikuwa linamnyima sana nguvu ya kusema.” Mbunge huyu ni wa mfano wa kuigwa kwa jinsi anavyopigania maendeleo ya watu hasa watu wa Mkange. Sisi tutamuunga mkono na tuko naye na Mh. Rais ametuheshimisha Chama Cha Mapinduzi. Pia aliongeza kuwa hakuna shida mwaka huu tutashinda kwa ukubwa sana.”

Serikali imeendelea kutenga pesa za maendeleo katika halmshauri hiyo, ambapo zaidi ya Shilingi Bilion 130 za miradi mbalimbali zimepelekwa wilayani hapo zikiwemo fedha za Elimu, Maji, Barabara n.k
Posted by MROKI On Monday, February 10, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo