Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.
“Serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Vijana” amesema.
Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 29, 2024 Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana.
Aidha, amesema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Bi. Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.
0 comments:
Post a Comment