Nafasi Ya Matangazo

October 16, 2024

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Oktoba 15, 2024 amejiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kurakatika kituo kilichopo  Kitongoji cha Unyamwezini Kata ya Itumbili  Wilayani Magu mkoani Mwanza ikiwa ni maandalizi ya uchaguxi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, mwaka huu.

Mara baada ya kuwasili katika Kituo cha kuandikisha wapiga kura katika orodha ya mtaa huo ,Waziri Tax alilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nasari na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Magu Bw. Mwagala Charles Masunga na baada ya kujiandikisha, Waziri Tax akatumia wasaa huo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Joshua Nasari kwa kazi nzuri anayoifanya katika uandikishaji huu wa daftari la makazi la wapiga kura katika Serikali za mitaa kwenye Wilaya ya Magu.

Pia Mhe. Waziri akasema kuwa taarifa aliyopewa na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Magu Bw. Mwagala  Masunga inatia moyo sana, kuongeza "kama tunavyofahamu wote Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifungua  zoezi hili kuonesha umuhimu wake tarehe 11 Oktoba, 2024 ambayo ndiyo siku alijiandikisha huko Dodoma ambako ndiyo makazi yake, na ndiyo maana na mimi nimekuja Wilayani Magu kujiandikisha ambapo ndiyo makazi yangu.

Aidha, Waziri Dkt. Tax akasisitiza kuwa amefurahi sana kupata fursa ya kujiandikisha pia akatoa wito kwa Wana Magu wenzake na wananchi  wote nchini kwenda kujiandikisha kwani hili ni zoezi muhimu sana nchini  na akasisitiza kuwa uongozi unaanzia kwenye maeneo yetu tunayoishi tusipojiandikisha katika daftari la kupiga kura la mkazi tutakosa fursa ya kuchagua viongozi  watakaokuletea maendeleo.

Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kama mlivyojionea wakati Mwenge wa Uhuru tulivyoupokea hapa Magu  ukizindua miradi mbalimbali ya maendeleo miradi hiyo imetokana na Uongozi bora wa Mheshimiwa Rais Samia ambaye ameonyesha njia lakini huku kwetu chini kuna DC na Mkurugenzi wa Halmashauri ambao hawawezi kufanya kazi peke yao lazima tuchague viongozi makini watakaosaidiana nao kutuletea maendeleo.





Posted by MROKI On Wednesday, October 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo