Nafasi Ya Matangazo

September 01, 2024

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 01 Septemba 2024 katika kikao chake maalum, imefanya uteuzi wa majina ya wana-CCM 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kati ya wanachama 47 walijitokeza kuwania uteuzi huo.

Wanachama walioteuliwa na Kamati Kuu ni hawa wafuatao:
1. Ndugu Gladness Ladislaus SALEMA
2. Ndugu Maria Alphonce SEBASTIAN
3. Ndugu Queenelizabeth William MAKUNE
4. Ndugu Ester Anania CHAULA
5. Prof. Neema Penance KUMBURU
6. Ndugu Lucia Sebastian PANDE
7. Ndugu Fatuma Abdallah KANGE
8. Ndugu Hawa Suleiman MKWELA
9. Ndugu Fatma Suleiman MSOFE
10. Ndugu Theresia Rosemary DOMINIC

Wagombea walioteuliwa, watapigiwa kura kesho Jumatatu, tarehe 2 Septemba 2024 na kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, saa 8 mchana, jijini Dodoma. Kisha tarehe 5 Septemba 2024, kutakuwa na uchaguzi wa kumpata mbunge mmoja kwa kuchaguliwa na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Kamati Kuu imewaondoa viongozi wawili kwenye nafasi zao kwa kukiuka maadili ya uongozi. Waliondolewa ni:

1. Palina Ninje, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Jumuiya ya CCM, Mkoa wa Lindi.
2. Abdul Rashid Zahoro, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.


Posted by MROKI On Sunday, September 01, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo