Nafasi Ya Matangazo

June 07, 2024



Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefungua maonesho ya Utalii ya  _Karibu Kili Fair_ yanayofanyika katika Viwanja vya Magereza Kisongo Mkoani Arusha na kuhamasisha wanachi kupigia kura vivutio  vya utalii vilivyoingia katika kinyang'anyiro cha tuzo la _World travel a_ wards kwa mwaka 2024.

Akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas, Mhe. Kairuki ametembelea banda la NCAA na kujionea shughuli za utoaji elimu na maelezo kuhusu Utalii, uhifadhi na maendeleo ya Jamii zinazofanyika katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Katika banda la NCAA  Waziri Kairuki alitumia muda huo kuwahamasisha wageni waliotembelea maonesho hayo kupigia kura vivutio vya utalii ambapo eneo la hifadhi ya Ngorongoro linawania tuzo ya kuwa kivutio bora cha Utalii barani Afrika kwa mwaka 2024.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro lilishinda tuzo hiyo mwaka 2023 na mwaka huu linawania tuzo hiyo ambapo hatua za upigaji kura ni kama ifuatavyo 👇👇

1.Tembelea tovuti ya www.worldtravelawards.com/vote
2. Jisajili kwa kufuata hatua zote
3. Fungua Barua pepe yako uliyojaza ili kufanya uthibitisho

4. Chagua bara la Afrika, piga kura kwenye kipengele cha Africa’s Leading Tourist Attraction na chagua Ngorongoro Conservation Area

Kura Yako, Ushindi Wetu!
Posted by MROKI On Friday, June 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo