Nafasi Ya Matangazo

June 24, 2024






Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi wa uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza unao milikiwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia Kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited kwa asilimia 16 na Kampuni ya Perseus kutoka nchini Australia kwa asilimia 84.

Katika kikao hicho, Mahimbali ameipongeza Kampuni ya Persues Mining kwa wasilisho na taarifa iliyotolewa ambapo amewataka kuharakisha Mipango ya Kampuni hiyo ili mradi huo uweze kuanza kwa wakati.

"Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa wasilisho zuri na niwaombe kuharakisha taratibu na mipango yenu ili mradi huu uweze kuanza kwa wakati kama ilivyopangwa na pia napenda kusema kwamba mradi huu ni mradi mkubwa na muhimu kwetu hivyo, nisisitize kwamba mradi huu uanze haraka," amesema Mahimbali.

Naye, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga ameitaka Kampuni hiyo kuendelea na mipango wa utafiti na upembuzi yakinifu kwa ajili ya upanuaji wa mgodi huku shughuli za ujenzi wa mgodi zinaendelea kwa lengo la kuharakisha uzalishaji.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Persues Mining, Matt Cavedom amesema, mradi wa uchimbaji madini ya dhahabu wa Nyanzaga unatarajiwa kuanza shughuli za ujenzi wa mgodi huo Januari, 2025 na kukamilika ndani ya miezi 24 ambapo utakuwa na uhai wa miaka 10.7.

Pamoja na mambo mengine, Cavedom amesema Kampuni ya Sotta Mining imekamilisha masuala yote yaliyopo kwenye Sheria ya Madini likiwemo suala la Ushirikishwaji wa Jamii Sehemu za migodi (Local Content) pamoja na mpango wa ufungaji wa mgodi pinda watakapomaliza shughuli za uchimbaji (Mining Closure).

Katika hatua nyingine, Cavedom meiomba Serikali kusaidia michakato mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa vibali kutoka Tume ya Madini ili kuongeza eneo la uchimbaji wa chini kwa chini (underground mining).
Posted by MROKI On Monday, June 24, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo