Nafasi Ya Matangazo

May 19, 2024

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza   katika hafla ya utoaji tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kwa Tunza jijini Mwanza, Mei 18, 2024.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza   katika hafla ya utoaji tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kwa Tunza jijini Mwanza, Mei 18, 2024.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi, Khadija  Mfaume Liganga, tuzo ya mshindi wa jumla ya Malkia wa Nguvu  2024   katika hafla ya utoaji tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kwa Tunza jijini Mwanza, Mei 18, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Malkia wa Nguvu 2024   katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kwa Tunza jijini Mwanza, Mei 18, 2024. Waliokaa kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa  Mwanza, Michael Lushinge, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, Mkurugenzi wa Cloud Media , Sheba Kusaga na Naibu Waziri  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi.  
******************
🔴Awataka watumie taarifa za na takwimu za sensa kuandaa mipango yao
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wanaotekeleza afua mbalimbali za wanawake watumie taarifa na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika kuandaa mipango na mikakati ya uwezeshaji wa wanawake nchini.

Mbali na hayo pia Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza wadau hao wanaotekeleza afua za wanawake waandae mipango yao kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali. “Hii ni namna bora ya kuharakisha ustawi na maendeleo ya wanawake.”

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo jana (Jumamosi, Mei 18, 2024) katika hafla ya utoaji wa tuzo ya Malkia wa Nguvu iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Kwa Tunza Beach jijini Mwanza.

Pia, Waziri Mkuu amesema kuanzia Julai 2024 Serikali itatoa utaratibu wa namna ya uendeshaji na utoaji wa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

“Nitoe rai kwa wanawake wote na makundi ya vijana na watu wenye ulemavu wazingatie utaratibu utakaotolewa na niwakumbushe kuwa fedha inayotolewa ni mikopo siyo ufadhili hivyo wanufaika wote wawajibike kuirejesha.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutoa kipaumbele katika masuala ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa makundi maalum ya wanajamii likiwemo kundi la Wanawake.

Amesema Serikali kwa mwaka 2023/2024 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 18.5 kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo kwa riba ya asilimia saba na kufanya makubaliano na NMB yatakayowezesha wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wanawake kupata mikopo yenye riba nafuu. 

“Ninafuraha sana kwa kuwa hamasa inayotokana na ushiriki wa Tuzo ya Malkia wa Nguvu imeendelea kuwavuta wanawake wengi zaidi na kuwafanya waongeze ubora wa shughuli wanazozifanya sambamba na kukuza biashara zao.”

Amesema anafahamu kuwa moja ya malengo ya Mradi wa Malkia wa Nguvu ni kuimarisha fursa za ajira na kuwa kichocheo muhimu cha uzalishaji wa ajira mpya. “Ninawapongeza sana kwa kuchangia jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana.”
Posted by MROKI On Sunday, May 19, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo