Wito huo
umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.
Kamilembe Mutasa wakati akifungua mafunzo kuhusu utekelezaji wa Itifaki ya
Montreal inayohusu Kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni leo Mei 06, 2024 jijini
Dar es Salaam.
Amesema lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa mafundi hao kuhusu matakwa ya itifaki hiyo ambapo
wanasayansi walivumbua kemikali hizo mwanzoni mwa miaka ya 1970 ambazo
hujipenyeza angani na kumong’onyoa tabaka la hewa ya ozoni kwa kuruhusu mionzi
au miale ya jua kufika katika uso wa dunia na kusababisha madhara kwa afya ya
binadamu na mazingira.
Bi. Kemilembe
ametaja madhara hayo kuwa ni magonjwa ya saratani ya ngozi, uharibifu wa macho
unaosababisha upofu na athari kwa ukuaji wa mimea na viumbe hai wengine.
Amesema kemikali
zinazoharibu tabaka hilo zinatumika katika majokofu na viyoyozi, vifaa vya
kuzima moto, usafishaji chuma, utengenezaji magodoro, ufukizaji wa udongo
katika vitalu vya tumbaku na kilimo cha maua na hifadhi ya nafaka katika
maghala.
Kutokana na
changamoto hiyo, Bi. Kemielembe amesema juhudi zimeendelea kufanyika tangu mwaka
1985 baina ya Serikali kitaifa na kimataifa kukubaliana kuanzisha Mkataba wa
Vienna na Hifadhi ya Tabaka la Ozoni na hatimaye Itifaki ya Montreal kuhusu
udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni ambapo shabaha yake kuu
ni kusitisha utengenezaji na utumiaji wa kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la
Ozoni.
Ameongeza kuwa Itifaki
ya Montreal imekuwa ikifanyiwa marekebisho mbalimbali kutokana na tafiti
zinazoainisha kemikali mbalimbali zinazomong’onyoa tabaka la ozoni au kuwa na
athari zingine za kimazingira kama kusababisha ongezeko la joto duniani.
Hivyo, mafunzo hayo yanayohusu njia bora za kuhudumia vifaa ikiwemo majokofu na viyoyozi pasipo kuathiri mazingira yanatolewa na Mtaalamu wa Kimataifa wa viyoyozi na majokofu kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa la Mazingira (UNEP) Bw. Freeborn Taruvinga kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Bagamoyo Mhandisi Goodluck Rulagora pamoja na Bw. Said Mziwanda koka kutoka Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Chang’ombe, jijini Dar es Salaam chini ya shughuli wezeshi ya kujenga uwezo wa kitaasisi katika kutekeleza Itifaki ya Montreal inayotekelezwa na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
0 comments:
Post a Comment