Fedha za
Mfuko wa Jimbo zimeendelea kuleta tija na matokeo chanya katika kuimarisha na
kukuza uchumi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla na hivyo
kuleta manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano.
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas
Katambi amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Wingwi Mhe. Omar Issa
Kombo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingir) Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo tarehe 06 Mei, 2024 bungeni.
Katika swali
lake Mhe. Kombo alitaka kujua lini Serikali itafanyia kazi changamoto ya Kodi
na Tozo kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa upande wa Zanzibar, Naibu Waziri
Katambi amesema kuwa kodi na tozo hutozwa kwa mujibu wa Sheria pindi bidhaa au
huduma zinapotolewa au kununuliwa.
Aidha, amebainisha
kuwa bidhaa na huduma zinazotolewa hukatwa kodi ya zuio la kodi (With Holding
Tax) kwa kuzingatia Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332 chini ya kifungu cha
83 (1) (c) kwa malipo ya ada ya kwa huduma kwa ajili ya utoaji wa huduma ya
kitaalamu na kifungu (83 A) malipo kwa bidhaa zinazotolewa na mkazi wa
uendeshaji biashara.
Naibu Waziri
Katambi amesema kuwa kodi hutozwa kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi inayotumika
Zanzibar inayojulikana kama sheria zinazotolewa na mkazi wakati wa undeleshaji
biashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment