KAMPUNI ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Geita (GGML) imeishukuru Serikali kwa kutoa mazingira mazuri ya uwekezaji.
Akizungumza leo Mei 22, 2024 katika Jukwaa la Tatu la Uwekezaji katika Sekta ya Madini linaloendelea jijini Arusha, Mkuu wa Sheria kutoka
Kampuni ya AngloGold Ashanti - Geita Gold Mining Limited (GGML), David Nzaligo amesema kuwa kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita, mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji yameimarika na kuwa bora zaidi kwa kipindi kifupi.
Aidha amesema, katika kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wa kampuni hiyo mgodi umekuwa ukitoa fursa kwa wananchi ya kusambaza bidhaa sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya umeme na kuanza kutumia umeme wa TANESCO ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati ya mafuta.
Ameeleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kutoa ujuzi kwa watanzania ili kupata ajira ambazo hapo awali zilikuwa zinafanywa na wageni.
Jukwaa hilo la Ushirikishwaji Watanzania katika Sekta ya Madini limeanza rasmi leo, linafanyika kwa siku tatu likiwa na kauli mbiu 'Uwekezaji wa Bidhaa za Migodini kwa Maendeleo Endelevu'
Mbali na mijadala mbali mbali pia jukwaa hili la tatu linaambatana na maonesho mbalimbali ya kampuni za uchimbaji madini, watoa huduma kwenye migodi ya madini, Taasisi za Fedha na Serikali.
0 comments:
Post a Comment