Nafasi Ya Matangazo

April 09, 2024






Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K.Mmuya amefungua kikao kazi cha Wakuu wa Divisheni za utawala na Rasilimali watu katika Mamlaka za Serikali za mitaa kwa Mkoa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na utatuzi wa kero za wananchi.

Kikoa hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo April 09, 2024, kimegusia wajibu wa Maafisa Utumishi kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwani malalamiko mengi yanayotolewa wao ndio wanapaswa kutoa majawabu.

“Kauli mbiu ya ‘kero yako wajibu wangu’ iliyozinduliwa na Mkoa, inaongeza hamasa ya kututaka sisi watumishi kutatua kero za wananchi. Hii inadhihirisha Utashi na nia njema ya dhati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule katika kuhakikisha wananchi wanapewa kipaumbele kwa mambo yanayowatatiza.

Katibu Tawala huyo amesisitiza juu ya matumizi ya kauli mbiu hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

“Kila mtu atatumia kauli mbiu hiyo kutuongoza watumishi wote, viongozi, wadau wa ndani ya Mkoa wenye dhamira na nia ya kuona kila mmoja anaunga Mkono Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kupunguza changamoto za wananchi wa kawaida kwani hao ndio kupaumbele cha Serikali yake”. Ameongeza Bw. Mmuya.

Hata hivyo, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Dodoma Bi. Coletha Kihwale amesema kikao kazi hicho kitasaidia kukuza kaulimbiu hiyo yenye msingi wa kuanzisha kampeni ya kukuza ustawi kwa wanachi na Serikali yao na kuhimiza uwajibikaji kwa wanachi na viongozi.
Posted by MROKI On Tuesday, April 09, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo