Nafasi Ya Matangazo

April 08, 2024









Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefungua kikao cha kwanza cha Kamati kuu ya Kuratibu Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima maarufu kama Nane nane kwa Kanda ya kati ambapo Mwaka huu (2024) zinatarajiwa kufanyika kitaifa kwenye Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na wajumbe walioshiriki kikao hicho kwenye ukumbi wa ofisi yake jengo la Mkapa Jijini Dodoma, Mhe. Senyamule amewataka washiriki hao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwenye Jukumu lolote watakalopangiwa ili kuondoa sintofahamu kuelekea kilele cha siku hiyo.

“Kila mtu ni vema atimize wajibu wake, usingoje hadi uambiwe nini cha kufanya. Kitu chochote kinachotakiwa kufanyika kifanyike ili Maadhimisho hayo yaweze kuwa na tija kama inavyotarajiwa na ukizingatia ni sherehe ya Kitaifa ambayo itajumuisha mambo mengi katika hizo siku kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mwisho.

“Kila mmoja awe sehemu ya maadalizi ili  kuhakikisha lengo letu linatimia kwa Kiwango kile tunachokitarajia katika sherehe hizi za Kanda ya Kati mwaka 2024" Amesema Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amesema kikao hiki kitaonesha Dira wapi tumetoka na tunapoelekea na kuna mambo hayatakiwi kusubiri na kupoteza muda. Kila timu iliyopangwa ihakikishe inafanya vizuri ili kuondoa sintofahamu hapo mbeleni.

Vile vile Bi. Aziza Mumba, Katibu Tawala Msaidizi sekta za Kilimo na Uchumi Mkoa wa Dodoma amesema kila mwaka Agosti Mosi hadi 08, Serikali hufanya sherehe za Nane Nane kikanda na sherehe za maonesho mahususi ya wakulima.

"Mikoa ya Singida na Dodoma inayounda Kanda ya Kati, kupitia sherehe hizi ina lengo la kutangaza fursa za uwekezaji, biashara sanjari na kusambaza taarifa za teknolojia na mbinu za Kilimo bora zinazoweza kuwawezesha wakulima kufanya kilimo cha kisasa na kupata mazao stahiki" Bi Mumba.

Kikao hicho kimeazimia mambo kadhaa ikiwemo; kamati ndogo ibainishe na kuongeza taasisi za Wizara ya Kilimo na Misitu, Taasisi za Misitu zihusishwe ipasavyo kwani Sekta ya Kilimo inahusisha Mazao, Mifugo, Uvuvi, Madini na Misitu, kuweka Kongamano la siku moja la Uwekezaji litakaloangazia fursa za Sekta zote, Kamati ziundwe na kuridhiwa mapema, Uwepo wa Utalii wa kutembelea miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa, Mpango kazi uwe na muda wa utekelezaji n.k⁰⁰⁰⁰/
Posted by MROKI On Monday, April 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo